Tuesday, October 2, 2012

Ukimkosa Ric-Ross wiki hiii jinyonge..pata mwoneko, kifupi mwanaume wa ukweli ndani ya Dar


utamtakaaaaa.....
Na Mahmoud Zubeiry
SERENGETI Fiesta 2012, nani anayeifanya iwe na joto kali ile mbaya? Kuna ‘mnyamwezi’ mmoja mwenye midevu na mwili mkubwa, anayepiga Hip hop ya kigumu anakwenda kwa jina la Rick Ross. Nani mwingine? Ndiyo huyo.
Jamaa anatua Dar es Salaam keshokutwa kwa ajili ya show ya kilele cha Serengeti Fiesta 2012, kwenye viwanja vya Leaders Club, mwishoni mwa wiki.  
Akizungumzia ujio wa msanii mkubwa kama huyo katika mahijiano maalum jijini Dar es Salaam jana, meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo amesema tamasha la Serengeti Fiesta limekuwa likifanya vizuri sana katika mzunguko wake na kwamba watanzania wamekuwa wakifurahia uwepo wa tamasha hilo kutokana na mafanikio mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyapata kila ilipofika msimu  wa Serengeti Fiesta “mwaka huu tutakuwa na Rick Ross na kwamba watanzania waendelee kujenga imani na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager,  kwani kila kilele cha msimu wa tamasha hili ndio mwanzo wa maandalizi ya msimu unaofuata”.
Rick Ross ambaye ni mmoja kati ya wasanii wanaotamba sana katika miondoko ya kurap (hip hop) nchini marekani, atawasili hapa nchini siku ya alhamisi tayari kabisa kutumbuiza katika maadhimisho ya kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki hii.
Msimu wa Serengeti fiesta ulianzia katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Musoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Iringa ambapo wakazi wake walipata burudani na ladha ileile ya bia ya Serengeti kabla ya kufikia mwisho wa msimu wake wiki hii. 
Wasanii waliburudisha katika tamasha la Serengeti Fiesta nyanda za juu kusini ni pamoja na Inspector Haroun, Juma Nature, Roma Mkatoliki, Linah, Amini, Supa nyota Serengeti fiesta 2012 na wengine.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani wanatarijwa kumiminika katika viwanja vya Leaders Club kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa hapa nchini, kabla ya kilele cha msimu wa ‘BHAAAS’ kumaliziwa na msanii Rick Ross na kundi lake kwa kiingilo cha shilingi 20,000/= za kitanzania kwa wale watakaonunua tiketi zao mapema na elfu 25,000/= kwa wale watakaonunu tiketi getini.
Katika tamasha la Serengeti Fiesta msimu wa uliopita uliokuwa ukijulikana kama ‘Haina Majotroo’ Kampuni ya bia ya Serengeti iliwaleta wasanii maarufu ambapo msanii wa muziki wa raga ‘Shaggy’ alitumbuiza katika uzinduzi wa msimu huo jijini Mwanza na msanii nyota kutoka nchini Marekani Ludacris alihitimisha msimu wa kwa kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar Es Salaam na majirani zake kama kawaida katika viwanja vya Leaders Club.
Umaarufu wa tamasha Serengeti Fiesta umekuwa ukitengeneza ajira mbalimbali za muda mfupi na kudumu, na pia nyingine zikianzishwa kupitia Serengeti Fiesta katika maeneo yote ambayo tamasha hilo lilipata kupita zikiwemo kuibuliwa kwa wasanii chipukizi na baadaye kujitegemea kimuziki, kujengeka kwa majina ya wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika zaidi kwa mashabiki wa muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu kupitia tamasha hili la Serengeti Fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia ya Serengeti Premium Lager.     
HUYU NDIYE RICK ROSS:
Oktoba 14 mwaka jana, rapa Rick Ross alipata ugonjwa wa moyo mara mbili kwa siku moja, mara ya kwanza alipata shambulio hilo la moyo asubuhi kabla ya kurejea mara ya pili wakati wa jioni akiwa ndani ya ndege.
Rafiki wa karibu wa Ross alimtaarifu mpenzi wake kuwa moyo wa rapa huyo umesimama na wataalamu wanahangaika kuhakikisha hapotezi maisha.
“Madaktari hawajasema kama amekufa, hivyo bado tuna matumaini, tuendeleeni kumuomba Mungu,” anasema rafiki huyo, maombi hayo yalionekana kusaidia na hali kuwa nzuri.
Shambulio hilo la moyo la pili lilimpata jioni hiyo ya Oktoba 14 baada ya lile la kwanza la asubuhi, akiwa ndani ya ndege ya Delta Airlines, wahudumu wa ndege hiyo na rubani waliamua kutua kwa dharura Fort Lauderdale na kupatiwa matibabu katika hospitali ya uwanja huo wa ndege na hali yake kuwa nzuri, kisha kukodiwa ndege ya binafsi kuendelea na safari yake.
Mwenyewe alituma picha za video kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter, akisema kuwa hali yake iko sawa: “Niko sawa,” anasema rapa huyo.
Rick Ross, au The Boss jina lake halisi ni William Leonard Roberts II, alizaliwa Januari 28 mwaka 1976, eneo la Coahoma County, Mississippi nchini Marekani.
Jina la Rick Ross, alilipata kutoka kwa askari wa barabarani aliyekuwa akihusika na kudhibiti dawa za kulevya (Ricky Ross), ambapo alimshitaki rapa huyo na kulipwa dola milioni 10 kwa kutumia jina lake.
Kabla ya kupigwa faini ya dola milioni 10, Jay-Z alitakiwa kutoa ushahidi juu ya jina hilo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Def Jam, ambako Ross alikuwa ameingia mkataba wa kufanya kazi katika studio hiyo.
Baadaye alikataa taarifa za kuwa ana mpango wa kubadilisha jina hilo,  badala ya Rick Ross kuwa Ricky Rozay, kutokana na tatizo lililotokea la kupigwa faini, lakini alipinga vikali jambo hilo.
Baada ya kuingia mkataba na kampuni ya Suave House Records, iliyokuwa ikitumiwa na 8Ball & MJG, baadaye aliingia mkataba mwingine na Slip-n-Slide Records, iliyokuwa chini ya Def Jam tangu mwaka 2006.
Albamu yake ya kwanza aliitwayo Port of Miami iliachiwa Agosti mwaka 2006 na kushika nafasi za juu kwenye chati za Billboard kati ya albamu 200.
Albamu hiyo iliuza nakala 187,000 katika wiki ya kwanza, na kushirikishwa katika wimbo wa DJ Khaled Born-N-Raised na Holla at Me.
Machi mwaka 2008, alitoa albamu yake ya pili iliyoitwa Trilla, ambapo moja ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ilikuwa ni Speedin, aliyomshirikisha R. Kelly na kufanya vizuri.
Nyingine ilikuwa The Boss aliyompa shavu T-Pain ilishika nafasi ya 17 katika nyimbo 100, pamoja na Here I Am aliyofanya na Nelly na Avery Storm.
Katika kituo cha luninga cha MTV walimtaja kama rapa namba nne katika marapa 10,  katika kipengele chao cha Hottest MCs In The Game, huku akitoa ‘single’ yake ya This Is The Life akimshirikisha  Trey Songz.
Albamu ya Deeper Than Rap ilitoka mwaka 2009 na wimbo wa Valley of Death ulifanya vizuri katika albamu hiyo, kisha waliachia albamu nyingine ya Teflon Don Julai 6, mwaka 2010.
Wimbo uliofanya vizuri katika albamu hiyo ya Teflon Don ulikuwa ni Super High, akimshirikisha Ne-Yo na mwigizaji Stacey Dash akionekana kwenye video ya wimbo huo.
Kibao cha pili kilichoachiwa kutoka kwenye albamu hiyo ni Live Fast, Die Young, ambacho kilitayarishwa na rapa Kanye West, ambaye pia alishirikishwa na kushika nafasi ya pili katika chati za Billboard katika nyimbo 200 na kuuza nakala 176,000 kwa wiki ya kwanza.
Novemba mwaka 2010, rapa P Diddy alitangaza kupitia mtandao wa kijamii wa YouTube, kwamba anatarajia kufanya albamu ya pamoja na Ross ambayo itaachiwa mwaka 2011 na kibao kimoja cha Another One kiliachiwa katika mradi huo wa pamoja.
Nyota huyo alitangaza kuwa Desemba 13 mwaka huu, ataachia albamu ya God Forgives, I Don't,  lakini Novemba 17 mwaka huu,  alitangaza kusogeza mbele albamu hiyo hadi mwakani.
Ross alikamatwa na polisi akiwa na silaha na bangi Januari mwaka 2008, DJ Vlad alimfungulia kesi rapa huyo akimshutumu kumpiga.
Vlad anasema kuwa Ross alipanga ugomvi huo na watu wakampiga mjini Houston, Texas.
Machi 26 mwaka 2011, alikamatwa na polisi eneo la Shreveport akiwa na bangi, na taarifa ya polisi zilisema kuwa bangi hizo zilikutwa kwenye chumba chake.
Julai mwaka 2008, mtandao mmoja ulitoa taarifa kwamba Ross, alikuwa ofisa wa kukusanya mapato, mjini Florida, ikabandikwa picha yake akiwa amevaa sare za wakusanya mapato, lakini alikanusha na kusema picha hiyo haikuwa yake.
Baadaye Ross alikubali kuwa alikuwa akikusanya mapato miaka ya 90 katika mji huo wa Florida, hiyo ilitokana na kupatikana kwa ushahidi wa kutosha picha yake akiwa amevaa mavazi ya watoza ushuru na jamii kuiona picha hiyo.
Januari mwaka 2009, Ross alianzisha ugomvi na rapa 50 Cent, akisema Cent alimuangalia vibaya wakati wa onyesho la tuzo za BET,  lakini 50 Cent anasema hakumbuki kama alimuona Ross katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo.
Baadaye,  taarifa zilisema kuwa  Ross ‘alimchana’  Cent katika kibao chake cha Mafia Music, siku chache baadaye 50 Cent, aliachia kibao kiitwacho Officer Ricky (Go Head, Try Me), akimjibu Ross maneno aliyoyasema kwenye kibao cha Mafia Music.
Kabla ya 50 Cent kwenda Venezuela, aliachia video ya Warning Shot, ambayo alianza kwa kumponda Ross, katika mashairi ya wimbo huo, kisha baadaye 50 Cent aliachia katuni za Officer Ricky.
Februari mwa huo wa 2009, 50 Cent aliachia video nyngine akimfanyia mahojiano Tia, mama wa mmoja wa watoto wa Ross, ambaye aliweka wazi kuwa Ross alikuwa ofisa wa kukusanya ushuru na kuongeza kuwa maisha yake yote anayoishi ni ya uongo.
Alhamisi, Februari 5, mwaka 2009, rapa aitwaye Game, ambaye alikuwa na ‘beef’ na 50 kwa muda mrefu, akihojiwa kwenye kituo cha KUBE, akiulizwa kuhusu ugomvi wa wawili hao, alijibu kuwa mambo yanaonekana si mazuri kwa Ross.
Game aliamua kumsaidia Ross akianzia kwenye wimbo wa kwenye albamu ya Deeper Than Rap, wimbo wa In Cold Blood, ambapo video yake ilimuonyesha 50 Cent akiomboleza makaburini na Ross kutangaza amemaliza kipaji cha 50 Cent.
Ross alitoa wimbo mwingine Push ‘Em Over The Edge ‘akimdiss’ 50 Cent, ambaye na yeye aliachia video iitwayo A Psychic Told Me, akimponda DJ Khaled na Februari 12, 2009, alimjibu Ross na kibao cha Tia Told Me, akimshirikisha Lloyd Banks, alitoa nyingine kama Officer Down na Somebody Snitched.
Kwa muhtasari huyo, ndiye Rick Ross atakayefanya Serengeti Fiesta 2012 iwe taamu mpaka bhaaaaaas!
WASIFU WAKE:
JINA: William Leonard Roberts II
KUZALIWA: JanuarI 28, 1976 (35)
ALIPOZALIWA: Carol City, Florida, Marekani
KAZI: Muziki/Rapa
AINA YA MUZIKI: Hip hop, Mafioso Rap, Pop
ALBAMU ALIZOTOA:
2006: Port of Miami
2008: Trilla
2009: Deeper Than Rap
2010: Teflon Don
2012: God Forgives, I Don't [42]
from: http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment